CHAUREMBO NA KAULI NZURI KWA WAZAZI

 

Na, Emakulata Msafiri

Katika kijij kimoja alichokua anatawala mfalme mwenye nguvu nyingi jina lake lilijulikana kama Nguvu ni mali alibahatika kuzaa Watoto watatu, wakwanza ni wa kiume na wapili na watatu walikua ni wakike. Na majina yao yalikua hivi wakwanza aliitwa Kazumba, wapili Ndupele na watatu ambae pia ni wa mwisho Chaupele. Familia ya mfalme ilikua inaishi kwa amani na upendo laikini wanakijiji walikua hawana furahana kwasababu mfalme alikua anawaongoza kimabavu hasa ifikapo msimu wa mavuno wanakijiji wanalazimika kupeleka mazao yao yote kwa mfalme ili awagawie yeye na kiasi kikubwa na mazao anachukua yeye na kidogo ndicho anawagaia wanakijiji’

Kutokana na hali hiyo wanakijij wengi walikua wanakufa na njaa kali hasa watoto wadogo kwani hawawezi kuhimili njaa kwa kitambo kirefu. Siku moja mabinti wa mfalme walimuomba baba yao wakatembee maaneo mbalimbali ya Kijiji chao, baba tunaomba uturuhusu tukatembee maeneo yote ya Kijiji chetu tukaone watu wanavyoishi huko lakini hatuchelewi kurudi.

 Baba akasema lakini kuweni makini mnavyoenda huko maana kuna simba wakali baadhi ya maeneo, na Watoto wakajibu kwa furaha sawa baba tumekuelewa. Na safari yao ilianza mdogo mdogo kutembelea Kijiji chao katika matembezi yao walistaajabishwa na wanakijiji walivyokua wanaishi hasa Watoto, waliwaona Watoto wamevaa nguo chakavu tena zimechanika na wengine walikua wamevaa nguo za chini kama suruali na sketi lakini juu matumbo wazi.

 Wakaanza kusemezana wenyewe kwa wenyewe kwanini sisi tunaishi vizuri lakini wanakijiji anaowaongoza baba wanaishi mazingira magumu kama haya? Chaupele alimuuliza dada yake Ndupele, lakini cha kushangaza dada yake Chaupele alicheka kwa sauti kubwa na akasema mdogo wangu kuwa kama mtoto wa Tajiri, huoni kama sisi ni Watoto wa mfalme na hao ni Watoto wa maskini tena sio maskini tu wazazi wao ni wakulima na wanavaa nguo moja kila siku lakini sisi ni tunabadilisha nguo kila dakika na tunakula mda wote tunao jisikia.

Lakini Chaupele alianza kulia kwa huzuni na akasema dada yangu mbona unaroho mbaya hivi huoni kama hawa ni binadamu kama sisi na pia hicho chakula unachosema tunakula kila mda hujui kama Watoto hao wazazi wao ndio wanalima? Ndupele akamwambia mdogo wake naomba turudi nyumbani nisije nikakupiga maana akili zako zinawaza kama Watoto wa kimaskini.

Wakaanza safari yao ya kurudi nyumbani na walipofika walimkuta baba yao Pamoja na kaka yao Kazumba wamekaa sebuleni.Lakini mfalme alimpomuona binti yake mdogo aligundua hana furaha ikabidi amuite akae nae karibu amuuleze kinacho msibu. Binti yangu mbona umerudi huna furaha nani amekukere huko? Binti akajibu baba nimeona hali halisi wanakijiji wanavyoishi chakushangaza wanamaisha magumu lakini wewe unaewaongoza maisha yako mazuri.

Baba akajibu unataka niwafanyie nini binti wanakijiji ili uwe na furaha na usihuzunike sana?

 Mtoto akajibu wape uhuru kama unaotupa sisi Watoto wako.

Baba alivyosikia hivyo akaamuru wafanyakazi wake wote wapige mbiu kesho kutakua na mkutano kati ya wanakijiji na mfalme wao.

Basi kesho ilipofika watu walikusanyika kuitikia wito wa mfalme, mfalme akawauliza mnataka niwafanyie nini wanakijiji wangu ili tuishi kwa amani na upendo? Wanakijiji wakasema tunataka utujeengee vituo vya afya, shule na pia utuache huru katika mavuno yetu tutakua tunakugawia sisi wenyewe tukitaka. Na mfalme alikubali akasema saw ana wananchi waliondoka na furaha na tokea hapo Kijiji kilikua na maendeleo kedekede na binti Ndupele alijifunza upendo kutoka kwa mdogo wake Chaupele.

Hivyo tunajifunza kuwa:-

Tunatakiwa tuwe na upendo kama Chaupele na kauli nzuri za kuongea na wazazi wetu au wakubwa wetu tunapowaeleza jambo kama Chaupele na tusiwe na roho mbaya kama ya dada yake Chaupe ambae anaitwa Ndupele.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments