KUWEKEZA KATIKA WATOTO, TUNAJENGA MUSTAKABALI BORA KWA JAMII


Na, Emakulata Msafiri

Watoto ni sehemu muhimu ya jamii, kwani wao ndio viongozi wa kesho. Malezi bora na mazingira salama ni muhimu kwa ukuaji wao wa kimwili, kiakili, na kihisia. Wazazi, walezi, na jamii kwa ujumla wana jukumu kubwa katika kuhakikisha watoto wanapata elimu, lishe bora, na malezi sahihi ili kuwajenga kuwa watu wenye maadili na mchango mzuri kwa jamii.

Pia, ni muhimu kuwalinda watoto dhidi ya changamoto kama vile unyanyasaji, utapiamlo, na ukosefu wa fursa za elimu. Serikali na mashirika mbalimbali yanapaswa kushirikiana ili kuhakikisha haki za watoto zinalindwa na wanapata mahitaji yao ya msingi.


Haki za watoto ni zile haki za msingi ambazo kila mtoto anapaswa kufurahia ili kuhakikisha ustawi wake, maendeleo yake, na ulinzi wake. Haki hizi zimetajwa katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Mtoto (UNCRC) na zinaungwa mkono na sheria nyingi za kitaifa, kama vile Katiba ya Tanzania, Kenya, na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Haki za watoto ni pamoja na:

Haki ya kuishi na kuendelea , Kila mtoto ana haki ya kuishi na kupata huduma muhimu za afya na lishe Bora ambayo itasaidia kukua kwa ustawi mzuri na afya Bora na Haki ya kupata elimu Watoto wanapaswa kupata elimu bora bila ubaguzi.

Pia haki ya ulinzi dhidi ya unyanyasaji , Watoto wanapaswa kulindwa dhidi ya ukatili, unyanyasaji wa kimwili, kihisia, au kingono mfano mtoto Hana haki ya kuhojiwa na vyombo vya habari ikiwa hajapata ruhusa kutoka kwa wazazi wao.

Mtoto ana Haki ya jina na utaifa, Kila mtoto ana haki ya kusajiliwa kwa jina lake na kuwa na utaifa hii itasaidia kujulikana na watu na pia atatumia katika ngazi mbalimbali za elimu na itasaidia kupata kazi.

 Haki ya kupewa malezi na wazazi au walezi, watoto wanastahili kukua katika mazingira salama na yenye upendo pamoja na haki ya afya ya akili kwa kupata huduma za afya Bora, chanzo na lishe nzuri

Haki ya kushiriki na kutoa maoni, Watoto wana haki ya kusikilizwa na kushiriki katika maamuzi yanayowahusu kwa mfano kujieleza kwa Mambo mbalimbali yanayowakabili katika jamii inayowazingukaa.

Haki ya ulinzi dhidi ya ajira ya watoto – Watoto hawapaswi kulazimishwa kufanya kazi hatari au zinazoweza kudhuru maendeleo yao kwa kuangalia kunamaeneo mbalimbali watoto wanalazimishwaa kufanya kazi mfano kuosha magari na kutembea bidhaa mtaani Ili wapate hela ya kuendesha familia

 Haki ya kucheza na kupumzika, Watoto wanapaswa kuwa na muda wa kucheza na kushiriki katika shughuli za burudani mfano kucheza rede, kuruka kamba na kucheza kombolela hii husaidia kuimarisha afya ya miwili na akili.

Haki ya faragha, watoto wanapaswa kulindwa dhidi ya uingiliaji wa maisha yao binafsi bila sababu za msingi na pia haki hizi zinaweka msingi wa kuhakikisha watoto wanalelewa katika mazingira salama, yenye upendo, na yanayowawezesha kufikia ndoto zao.


Mwanakwetu Upoo?
Kumbuka tu,

Kwa kuwekeza katika watoto, tunajenga mustakabali bora kwa jamii nzima. Kila mtoto anapaswa kupata nafasi ya kukua katika mazingira yenye upendo, usalama, na fursa za maendeleo.

Nakutakia Siku Njema 

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments