SAFARI YENYE TUMAINI CHUNGU

Na, Emakulata Msafiri

Kulikuwa na kijiji kidogo kilichozungukwa na milima na misitu yenye kijani kibichi. Katika kijiji hicho, alikuwepo mvulana mdogo aitwaye Juma. Juma alikuwa na ulemavu wa miguu na alitumia magongo kutembea. Ingawa alikuwa na ndoto kubwa, watoto wengine walimdhihaki na mara nyingi hakuruhusiwa kushiriki michezo yao.

Mara nyingi mvulana huyo Alimpenda kujifungia.ndani na kulia sana kwani alijiona kabisa Hana nafasi ya kuishi kulingana na changomoto anazopitia kutokana na ulemavu wake unasumbua kwa miaka mingi na kunawakati alitamani kufa kutokana na Hali anazopitia ya kutengwa na watoto wenzie.

Mara nyingi wazazi wake walipenda kumsifia na kumtia moyo na kumwambia ni mtoto mzuri sana na ipo siku ndoto zake zitatimia kikubwa ni kusoma kwa bidii na kumsikiliza mwalimu kwa umakini pindi anavyofundisha.


Na katika masomo yake kijana Juma alikua anajitahidi.sana na walimu walitokea kumpenda kutokana na tabia yake ya usikivu darasani na pamoja na nidhamu kwa walimu wake na alipata zawadi mbalimbali kwa kuongoza Kila mitihani inapokuja.

Siku moja, mwalimu mpya aliyeitwa Bi. Amina alifika kijijini. Alipogundua jinsi Juma alivyotengwa, aliamua kufanya mabadiliko. Alianzisha shindano la sanaa na muziki shuleni, akisema, "Ushindi haupatikani kwa mbio tu, bali kwa vipaji mbalimbali."

Juma, aliyependa kuchora, alitumia muda wake mwingi kuchora picha nzuri zilizoelezea maisha ya kijijini. Siku ya shindano ilipofika, kila mtu alistaajabu kazi yake. Hakika, alitangazwa mshindi wa kwanza! Watoto waliokuwa wakimcheka hapo awali walimpongeza na hata kuomba kujifunza kutoka kwake.


Na kijana Juma aliwasaidia wenzake kujifunza kuchora na walimkubali sana kwani alikua sio mbinafsi katika kujifunza ndipo watoto walimpongeza sana Juma na walitaka kujifunza vitu vingi kutoka kwake ikiwemo na mambo ya taaluma.

Baada ya siku hiyo, kijiji kilianza kuona thamani ya kila mtoto, bila kujali hali yake. Juma alizidi kung’aa, na ndoto zake zikawa nuru kwa wengine.

Mwanakwetu Upo!

Kila mtoto ana thamani yake na kipaji chake, na jamii inapaswa kuwapa wote nafasi ya kung'ara.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872




0/Post a Comment/Comments