Na, Emakulata Msafiri - Iringa
Hapo zamani za kale sungura na fisi walikua marafiki sana na waliishi kwa upendo sana.Nakatika maisha ya urafiki wao waliipangiana namna ya kutafuta chakula na waliazimia kusema kuwa kila mmoja atatafuta chakula kwa siku moja moja.
Basi ikaanza zamu ya fisi akaenda msituni akatafuta chakula akajanacho wakala wote kwa Pamoja na furaha tele,kesho yake ikafika zamu ya sungura kutafuta chakula akenda kutafuta na na hakurudi na chakula na siku hii wakalala njaa kwa sababu ya kukosa chakula.
Kesho yake ilipofika ilikua zamu ya fisi kutafuta chakula kaenda tafuta na akarudi na chakula tena alifanikiwa kupata mnyama wa mwituni aliyekufa, basi aliporudi nyumbani sungura alimpokea kwa bashasha sana na akasema kuwa.
Rafiki yangu na kupenda sana kwasababu ni mjanja na unapata chakaula kila siku na baada ya kusema hayo alimkumbatia kwa nguvu. Basi fisi akasema kupata chakula msituni sio kazi rahisi inabidi ujitoe sana maana kunatisha sana kule msituni.Basi kesho yake ilipofika sungura alienda kutafuta chakula lakini hakupata kitu tena akarudi mikono mitupu wakalala njaa tena.
Basi usiku huo kwa upande wa fisi ulikua mrefu sana lakini sungura alilala fofofo huku akikoroma, fisi alijiuliza kimoyoni kwanini rafiki yangu sungura kila siku akienda kutafuta chakula hapati shida nini jamani lakini hakupata majibu ikabidi alale kwa kuweweseka maana alikua anahisi njaa sana.
Kesho iliipofika fisi ilikua zamu yake kutafuta chakula aliendaa misituni kutafuta, punde kidogo akamuona jirani yao kobe wakasalimia, na baada ya kusalimiana kobe akamuuliza fisi;Fisi Nikwanini unapeleka kila siku chakuala nyumbani na unakula na sungura? Fisi alishangaa hilo swali aliloulizwa na bwana kobe , lakini bwana kobe aliendelea na kusema mweinzio sungura akija msituni kutafuta chakula anapata na anakula huku huku kama huamini wewe mfatilie utagundua tu michezo yake.
Basi fisi alimshukuru sana bwana kobe na akaseama atafatilia kwa akenda zake nyumbani akiwa amebeba kitoweo, sungura alifurahi sana akala hadi mifupa. Kesho yake ilikua zamu yake kutafuta chakula na fisi alimfuata nyumanyuma ili ajue anachokifanya sungura.
Baada ya kufika msituni sungura alipata chakula na akaa chini anakula, hapohapo fisi akamfuma na sungura alishaangaa sana na alijisikia aibu akabaki ameinamisha kichwa chini hana la kusema nna fisi hakusema chochote baada ya kumuona akaondoka taratibu kwa huzuni akaelekea nyumbani akaanza kufungasha vilago vyake aondoke.
Mara kidogo anamuona sungura anakuja analia kwa uchungu lakini moyoni mwake ameejaa unafiki na usaliti. Akaanza kumuomba msamaha fisi ili waandelee kuishi wote, Sungura akasema naomba unisamahe rafiki yangu kipenzi ubinafsi wangu na tamaa zangu ndio zimeniponza lakini si rudii tena naomba unisamehe sana’
Lakini fisi hakujibu chochote akaendelea kujifungasha na akaondoka zake kuelekea Kijiji kingine kuishi kuendelea na maisha yake na sungura akabaki mpwekee. Ndio maana hadi leo sungura na fisi sio marafiki.
FUNDISHO
Katika maisha tusiwe wachoyo na wabinafsi kama sungura na tuwe na upendo kama wa fisi.
Nakutakia Siku Njema
Post a Comment