AFYA YA AKILI KWA WATOTO

 


Na, Emakulata Msafiri

 kulikuwa na mtoto mmoja aitwaye Tumaini ambaye siku zote alionekana mwenye huzuni na mpweke.

Mama yake alihisi kuna jambo, akajaribu kumwuliza, lakini Tumaini hakutaka kuzungumza. Kila siku alizidi kujitenga na marafiki zake. Wazazi wake waliamua kumpeleka kwa Mwalimu Neema, ambaye alikuwa mtaalamu wa watoto na afya ya akili.

Mwalimu Neema alimuuliza Tumaini maswali kwa upole na polepole mtoto akaanza kufunguka. Alisema kuwa alikuwa na hofu nyingi kuhusu masomo na alihisi kama hakuwa mzuri kama wenzake.


Mwalimu alimfundisha mbinu za kupunguza msongo wa mawazo, kama vile kupumua kwa kina, kuzungumza na marafiki na wazazi wake, na kufanya michezo inayompendeza. Pia, alifundishwa kuwa ni sawa kuhisi huzuni na muhimu kutafuta msaada.

Baada ya muda, Tumaini alianza kurejea kwenye hali yake ya kawaida. Alianza kucheka, kushiriki darasani, na kuwa na marafiki tena. Watoto wengine walipoona mabadiliko yake, walijifunza kuwa ni muhimu kuzungumza pale wanapokuwa na mawazo mazito.

Hii ilifanya kijiji cha Furaha kuwa mahali salama kwa kila mtoto, ambapo afya ya akili ilikuwa kipaumbele kwa kila mmoja.Ni muhimu kuzungumza kuhusu hisia zetu na kutafuta msaada tunapohisi huzuni au msongo wa mawazo.


emakulatemsafiri@gmail.com

 0653903872


0/Post a Comment/Comments