Na, Emakulata Msafiri
Haki ya kufanya kazi kwa watoto ni suala linalozingatiwa kwa umakini katika sheria za kitaifa na kimataifa ili kuhakikisha kuwa watoto wanalindwa dhidi ya unyonyaji na kazi hatarishi. Haki hizi zinajumuisha:
Haki ya Kulindwa dhidi ya Ajira ya Watoto, Watoto hawapaswi kulazimishwa kufanya kazi zinazoweza kuathiri afya, maendeleo, au elimu yao kwa mfano watoto hawaruhusiwi kutembeza vitu barabarani na mda huo anaetakiwa aende shule akapate elimu kwa manufaa ya baadae.
Haki ya Elimu, Watoto wanapaswa kupata elimu bora bila kulazimika kufanya kazi zinazoweza kuathiri masomo yao na kusababisha kuacha shule na kuwa watoto wamtaani au ombaomba.
Umri wa Kuanza Kazi, Sheria nyingi huweka umri wa chini wa ajira (kwa mfano, miaka 14 au 15 kwa kazi nyepesi na miaka 18 kwa kazi hatari). Lakini wazazi wengi au walezi wanawapa kazi ambazo haziendani na umri wao na kusababisha mda mwingine watoto kupoteza afya ya akili.
Haki ya Kufanya Kazi Salama, Ikiwa mtoto anafanya kazi (katika hali zinazokubalika), anapaswa kufanya kazi isiyo hatarishi kwa afya yake ya kimwili na kiakili na hii itasaidia mtoto kukua katika afya nzuri.
Kulindwa dhidi ya Ajira za Kulazimishwa, watoto hawapaswi kulazimishwa kufanya kazi kwa masharti mabaya au ya utumwa mfano kumlazimisha mtoto kuosha magari au kutembeza bidhaaa mbalimbali pembezoni mwa barabara.
Mikataba ya kimataifa kama Mkataba wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Mkataba wa Haki za Mtoto wa Umoja wa Mataifa (CRC) inasisitiza ulinzi wa watoto dhidi ya ajira hatari. Serikali, waajiri, na jamii wanapaswa kuhakikisha kuwa watoto wanapata haki zao bila kunyanyaswa au kunyimwa fursa za maendeleo.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment