NDOTO YA BONDIA MDOGO

 


Na, Emakulata Msafiri

Juma alikuwa mtoto mwenye ndoto kubwa ya kuwa bondia maarufu. Kila siku baada ya shule, alijificha nyuma ya nyumba na kufanya mazoezi ya kupiga ngumi kwenye mfuko wa mchanga aliotengeneza mwenyewe.

Siku moja, mzee Rashid, bondia wa zamani wa kijiji chao, alimwona Juma akifanya mazoezi. “Unapenda ndondi?” aliuliza kwa tabasamu.

“Ndio, nataka kuwa bondia shujaa!” Juma alijibu kwa msisimko.


Mzee Rashid aliamua kumfundisha mbinu sahihi za ndondi. Alimwonyesha jinsi ya kusimama vizuri, kujikinga, na kupiga ngumi kwa nguvu na ustadi. Juma alifuata mafunzo hayo kwa bidii, huku akijifunza kuwa mchezo wa ngumi siyo tu nguvu, bali pia akili na heshima.

Baada ya miezi kadhaa ya mazoezi, mashindano ya ndondi kwa watoto yalitangazwa kijijini. Juma alijiandikisha kwa ujasiri. Siku ya pambano, alisimama ulingoni akiwa na hofu kidogo, lakini alikumbuka mafunzo ya mzee Rashid. Alipigana kwa nidhamu na hatimaye akashinda pambano lake la kwanza!


Watu wote walimshangilia, na mzee Rashid alimwambia, 
“Umeonyesha kuwa bondia wa kweli siyo yule anayepiga kwa nguvu, bali anayepigana kwa moyo na akili.”

Juma alitabasamu, akijua kuwa hii ilikuwa tu hatua ya kwanza kuelekea ndoto yake kubwa ambayo alikua anatamani mda mrefu.

Lakini pia mchezo wa ngumi (boxing) ni mchezo maarufu wa kupigana unaohitaji nguvu, ustadi, na nidhamu kali. Ingawa ni mchezo wa kusisimua na wenye manufaa kwa mwili, una madhara kadhaa, hasa kwa afya ya mchezaji. Madhara haya ni pamoja na:


Majeraha ya kichwa, Ngumi zinazopigwa kichwani zinaweza kusababisha mtikisiko wa ubongo (concussions) na matatizo ya muda mrefu kama ugonjwa wa encephalopathy wa wapiganaji (CTE).

 Kupoteza fahamu,Pigo kali linaweza kusababisha mpiganaji kupoteza fahamu, jambo ambalo linaweza kuwa na madhara makubwa kwa afya ya ubongo na pia majeraha ya macho kwasababu ya kupigwa mara kwa mara usoni kunaweza kusababisha matatizo kama uoni hafifu au hata upofu.


emakulatemsafiri@gmail.com

065390387


0/Post a Comment/Comments